John 18:39-40

39 aLakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi’?”

40 bWao wakapiga kelele wakisema, “Si huyu mtu, bali tufungulie Baraba!” Yule Baraba alikuwa mnyang’anyi.

John 19:1-4

Isa Ahukumiwa Kusulubiwa

(Mathayo 27:15-31; Marko 15:6-20; Luka 23:13-25)

1 cNdipo Pilato akamtoa Isa akaamuru apigwe mijeledi. 2Askari wakasokota taji ya miiba, wakamvika Isa kichwani. Wakamvalisha joho la zambarau. 3 dWakawa wanapanda pale alipo tena na tena, wakisema, “Salamu! Mfalme wa Wayahudi!” Huku wakimpiga makofi usoni.

4 ePilato akatoka tena nje akawaambia wale waliokusanyika, “Tazameni, namkabidhi Isa kwenu kuwajulisha kwamba mimi sikumwona ana hatia.”
Copyright information for SwhKC